Featured
Loading...

WCF, ILO ZATOA MAFUNZO KWA MADAKTARI 380 JUU YA NAMNA YA KUTATHIMINI AJALI NA MAGONJWA YANAYOTOKANA NA KAZI

MAAJABU YA MTANDAONI BOFYA HAPO CHINI HUTAAMINI MACHO YAKO =>
MFUKO wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) kwa kushirikiana na Shirika la Kazi Duniani (ILO) wameanza kutua mafunzo kwa madaktari nchi nzima kuhusu namna ya kubaini na kushughulikia wahanga wa ajali na magonjwa yanatosababishwa na kazi. Jumla ya madaktari 380 wa hospitali za rufaa mikoani na wilayani watafaidika na mafunzo hayo.

Wataalamu kutoka ILO waliobobea katika ajali na magonjwa yanayotokana na kazi Dkt. Jacques Pelletier (kulia) na Dkt. Sylvie Thibaudeau wakibadilishana mawazo muda mfupi kabla ya kutoa mada zao.
Mafunzo yatatolewa kwa siku tano katika vituo vikubwa vinne ikiwemo Dar es salaam, Arusha, Mwanza na Mbeya. Wataalamu kutoka ILO waliobobea katika ajali na magonjwa yanayotokana na kazi Dr. Jacques Pelletier na Dr. Sylvie Thibaudeau ndio watakaoendesha mafunzo hayo.

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi Bw. Masha Mshomba amesema kwamba mafunzo haya ni hatua muhimu sana kwa Mfuko kwani Mfuko unaanza rasmi ulipaji wa mafao tarehe 01 Julai 2016 kwa Wafanyakazi wote watakaopata ajali au magonjwa kutokana na kazi.


 Bi. Isaka na Masha wakiwa kwenye meza kuu wakiandaa hotuba zao

 Miongoni mwa mafao yataayotolewa ni Huduma ya matibabu, Fidia kwa ulemavu wa muda, Fidia kwa ulemavu wa kudumu, Ukarabati na ushauri nasaha, Malipo kwa anayemhudumia mgonjwa, gharama za mazishi endapo mfanyakazi atafariki na fidia kwa wategemezi endapo mfanyakazi pia atafariki.

Bw. Masha Mshomba akifafanua dhumuni kubwa la kufanya haya mafunzo alisema, “Kazi kubwa ya madaktari hawa itakuwa ni kufanya tathimini ya magonjwa yanayotoka na kazi na kutupa ushauri wa kuendelea na malipo kama wahusika watakuwa wamepata ajali au kuugua na wakapata ulemavu” [1.6MB]VIDEO CHAFU YA WANACHUO WA UDSM YAVUJA IONE HAPO CHINI =>

UNGANA NASI FACEBOOK KWA KULIKE PAGE YETU

[1.6MB]HIZI NDIZO NJIA RAHISI ZA KUMRIDHISHA MSICHANA WAKO ZIONE HAPO CHINI =>

Chapisha Maoni

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright MFUKUNYUZI | Designed By Code Nirvana
Back To Top