Chama cha Wananchi CUF kimepanga kuiomba Mahakama ya Kimataifa uhalifu ICC kuanzisha uchunguzi dhidi ya viongozi wenye dhamana mbalimbali waliohusika kuchochea,kutoa na kusimamia maagizo yalipelekea makosa ya uhalifu wa kibinadamu yakiwemo yanayolenga wananchi na makundi ya watu.
Akizungumza katika uzinduzi wa ripoti ya uvunjani wa haki ya binadamu unaofanywa na vyoimbo vya dola dhidi ya wapinzani kwa mwaka 2015-2016, Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar Bw.Nassor Mazrui amesema chama hicho baada ya kuzindua ripoti hiyo kimepanga kuchukua hatua tano ikiwemo pia kufungua kesi katika Mahakama Kuu Tanzania dhidi ya Waziri wa mambo ya ndani ya nchi na Mkuu wa Jeshi la Polisi kwa ukiukwaji wa haki za binadamu.
Ripoti ya uvunjaji wa haki ya binadamu unaofanywa na vyombo vya dola dhidi ya wapinzani kwa mwaka 2015-2016,imeonyesha katika kipindi hicho watu 300 waliwekwa rumande,watu 200 walijeruhiwa,watu 13 kudhalilishwa kijinsia ambapo watu zaidi ya 70 walivunjiwea majengo,watu 3 walipata ulemavu kutokana na matukio hayo na 40 walihama makazi yao kukimbia vurugu za jeshi la Polisi.
UNGANA NASI FACEBOOK KWA KULIKE PAGE YETU
Chapisha Maoni