Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kupitia taarifa ya habari ya TBC, imetoa adhabu kwa Clouds TV baada ya kupokea malalamiko mengi kutoka kwa wananchi kuhusu kipindi hicho.
“Clouds Television inatakiwa kuwaomba radhi watazamaji wake na Watanzania kwa ujumla kutokana na kuwakwaza pamoja na kuwasababishia usumbufu kwa kurusha mada inayoongelea ushoga kwa namna ya upotoshaji kupitia kipindi cha Take One kulishorushwa tarehe 28 Juni 2016 . Taarifa ya kuomba radhi itoke siku tano mfululizo, kwenye taarifa zao za habari za saa moja na nusu usiku, na saa tano usiku kuanzia siku ya kusomwa hukumu ili na uthibitisho wa taarifa hizo uletwe Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania siku ya Jumatano tarehe 13 mwezi wa 7 mwaka 2016 kabla ya saa kumi jioni,” ilisema kamati ya maadili na mahudhi.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji Clouds TV, Bw. Ruge Mtahaba amesema kituo chake kitaendelea kusimamia maadili na kukemea vitendo vibaya katika jamii.
“Chochote kinachozungumzwa kuhusu maswala kama haya lazima kipigwe vita kwa namna yoyote ile, hakuna namna ya kuwa mbishi na kuingia kwenye vita ya vitu vidogo vidogo, na kama kukemea unakemea bila kunong’ona,” alisema Ruge. [1.6MB]VIDEO CHAFU YA WANACHUO WA UDSM YAVUJA IONE HAPO CHINI =>
UNGANA NASI FACEBOOK KWA KULIKE PAGE YETU
Chapisha Maoni