Waendesha mashtaka wa serikali Morogoro wamepewa miezi miwili kuwasilisha cheti kutoka kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) ili kuachia ama kuendelea kushikilia dhamana ya washtakiwa wanne wa kesi ya usambazaji wa picha chafu za ngono.
Washtakiwa hao ni wale waliopiga picha chafu za ngono dhidi ya mwanamke mmoja mkazi wa Kijiji cha Dakawa, Mvomero.
Mbele ya waendesha mashtaka wa serikali Gloria Rwakibalila, Edgar Bantulaki na Calistus Kapinga ilidaiwa mahakamani hapo na Ivan Msacky, Hakimu wa Mahakama hiyo kuwa, suala la dhamana chini ya Katiba ni haki ya kila mshtakiwa lakini akaonesha kushangazwa na upande wa mashtaka kutoeleza kwa uwazi sababu za kuendelea kuizuia dhamana hiyo.
Hakimu Msacky amewataka waendesha mashtaka hao kuhakikisha wanawasilisha mahakamani cheti kinachozuia dhamana kwa washtakiwa hao na sababu zake ili kesi hiyo iweze kuanza kusikilizwa.
Kesi hiyo ya jinai namba 54 ya mwaka 2016 inawakabili washtakiwa sita ambao ni Idd Adam Mabela, Zuberi Thabit, Rajab Salehe, Ramadhani Ally, Muksin Ng’ahy na John Peter ambao wanakabiliwa na shtaka la kusambaza picha chafu za ngono za msichana mwenye umri wa miaka 21 wilayani Mvomero mkoani humo. Washtakiwa wanaotaka dhamana ni mshtakiwa namba tatu hadi sita.
Hata hivyo, Hakimu Msacky jana aliahirisha kesi hiyo hadi tarehe 29 Juni mwaka huu ambapo kesi hiyo itaendelea kujadili suala la dhamana kwa washtakiwa hao.
Katika kesi hiyo iliyosikilizwa kwa mara ya kwanza tarehe 18 Mei mshtakiwa namba 1 na 2 wanatuhumiwa kumbaka na kumuingilia kinyume na maumbile msichana huyo Aprili 27, saa 1 usiku katika nyumba ya kulala wageni ya TITII iliyopo katika Tarafa ya Dakawa, Mvomero.
Katika kesi ya kwanza ya kubaka na kulawiti inayowakabili washtakiwa Mabela na Thabiti, wakazi wa jijini Mbeya ilishindwa kusikilizwa jana kutokana na wakili wa washtakiwa Mohamed Mkali kutokuwepo mahakamani.
[1.6MB]VIDEO CHAFU YA WANACHUO WA UDSM YAVUJA IONE HAPO CHINI =>
UNGANA NASI FACEBOOK KWA KULIKE PAGE YETU
Chapisha Maoni