Rais John Magufuli amemteua Prof. Ignas Aloys Rubaratuka kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) katika kipindi cha miaka mitatu kuanzia Mwezi Aprili mwaka huu.
Taarifa hiyo ilitolewa na Dk. Leonard Chamuriho, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano jana jijini Dar es Salaam.
“Kwa mujibu wa sheria Na. 17 ya mwaka 2004 ya Mamlaka ya Usimamizi wa bandari nchini rais Magufuli amemteua Pr. Rubaratuka ambaye alikuwa Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya TPA,” alisema Chamuriho.
Alisema kuwa Makame Mbarawa, Waziri wa Uchukuzi ameteuwa watu wanane kuwa wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) katika kipindi cha miaka mitatu.
“Aidha, Waziri mwenye dhamana ya sekta ya uchukuzi kwa mamlaka aliyopewa kwa mujibu wa kifungu Na. 6(2) cha sheria Na. 17 ya TPA ameteua watu nane kuwa wajumbe wa bodi ya wakurugenzi ya TPA,”amesema.
Alitaja wajumbe hao na vitengo vyao wakiwemo Jaffeer Mchano kuwa Mkurugenzi wa Mipango na Huduma wa Tanzania Investment Bank, Deusdedit Conatus Kakoko kuwa Meneja Miradi Tanroads.
Wengine ni Malata Pascal, Mkurugenzi Msaidizi, Division of Litigation and Abritration na Masanja Kungu Kadogosa kuwa kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL).
[1.6MB]VIDEO CHAFU YA WANACHUO WA UDSM YAVUJA IONE HAPO CHINI =>
UNGANA NASI FACEBOOK KWA KULIKE PAGE YETU
Chapisha Maoni