Mgeni Rasmi Tamasha la Ajira na Ujasiriamali Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano Mh Luhanga Mpina Akikagua Maonyesho ya Kazi Mbalimbali Kwenye Tamasha la Ajira na Ujasiriamali Lililofanyika Chuo Kikuu Mzumbe Mkoani Mbeya.
Katika kutengeneza Msingi Mzuri kwa Wanafunzi wake na kuwajengea uwezo Chuo Kikuu cha Mzumbe kampasi ya Mbeya kilifanya maonyesho makubwa ya Ajira na Ujasiriamali siku yatarehe 11 June 2015 mjini Mbeya. Tukio hilo la aina yake, pia lilishirikisha wanafunzi wa vyuo wingine vya nyanda za juu kusini.
Afisa Mtendaji Mkuu waEAG group Imani Kajula Akitoa Mada kwenye Tamasha La Ajira na Ujasiriamali Lililofanyika Mkoani Mbeya
Upatikanaji wa ajira za uhakika imekuwa changamoto kubwa sana kwa vijana wengi wanaomaliza vyuo Nchini Tanzania hivyo ujasiriamali ni njia moja muhimu ya kutatua changamoto hiyo.Wanafunzi wengi walioshiriki walieleza Furaha yao kwa Maonyesho hayo. Mgeni rasmi Mh.Mpina aliwataka Wanafunzi kutumia fursa zilizopo kujiletea Maendeleo na kujiajiri.
Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji Clouds Media Group Ruge Mutahaba Ambaye naye alitoa Mada Mbalimbali Namna ya Kukabiliana na Changamoto ya Ajira Hapa Nchini
Katika kufanikisha siku hiyo wataalam na wabobeaji wa biashara na fursa za ajira walialikwa kutoa mada na kushare uzoefu wao kwenye ujasiriamali na utendaji kazini. Watoa mada walio alikwa kwenye kongamano hili kubwani; Imani Kajula ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa EAG Group, Ruge Mutahaba ambaye ni Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji Clouds Media Group. Wakili Alberto Msando – Wakili maarufu wa kujitegemea na Mjasiriamali, Victor Kikoti Compliance Manager – LAPF na Ephraim Lwila – Meneja wa Tawi la CRDB Mbeya. Mgeni Rasmi wa Kongamano hilo alikuwa Naibu Waziri wa Mazingira na Muungano Mh.Luhaga Mpina.
Washiriki wa Tamasha Hilo wakisikiliza Kwa Makini Mda Mbalimbali Zilizowasilishwa Kwenye Tamasha la Ajira na Ujasiriamali Lililofanyika Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Mbeya
Pia katika kuhitimisha siku hiyo, Timu za wanafunzi wa Mzumbe Mbeya na TIA Mbeya walicheza Mechi ya mpira wa miguu, ambapo chuo cha Mzumbe kiliifunga TIA kwanjia ya penati. Mkurugenzi wa EAG Group Imani Kajula alikabidhi zawadi kwa timu zote mbili.
UNGANA NASI FACEBOOK KWA KULIKE PAGE YETU
Chapisha Maoni