Kamati ya haki, maadili na madaraka ya Bunge imemwita Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson kujieleza mbele yake kuhusu maombi yaliyowasilishwa na mbunge wa Simanjiro, James ole Millya (CHADEMA) kutaka kumwondoa madarakani.
Taarifa zilizopatikana baadhi ya wabunge Dodoma jana na kuripotiwa na gazeti la Mtanzania zilidai kamati hiyo tayari imemuhoji Dk. Tulia kuhusiana na suala hilo, habari zinasema Dk. Tulia alihojiwa na kamati hiyo ikiongozwa na mwenyekiti wake George Mkuchika ambayo endapo itaridhika kwa mujibu wa kanuni hoja hiyo itawasilishwa bungeni kwa ajili ya uamuzi wa bunge .
Alipoulizwa kuhusu lini kamati hiyo itakaa na kumhoji Dk Tulia mwenyekiti wa kamati hiyo George Mkuchika alisema haruhusiwi kuzungumzia shughuli za kamati hiyo kwa vyombo vya habari.
‘kamati yetu inafanya kazi kwa mujibu wa sheria, haturuhusiwi kusema nani kaitwa au kaandikiwa barua subirini kazi yetu inapokuwa tayari tunaiwasilisha bungeni‘ [1.6MB]VIDEO CHAFU YA WANACHUO WA UDSM YAVUJA IONE HAPO CHINI =>
UNGANA NASI FACEBOOK KWA KULIKE PAGE YETU
Chapisha Maoni