MSANII wa filamu Bongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’ amefunguka kuwa anajuta kutofunga ndoa na mkewe, Eva kwani anateseka sana kipindi hiki cha mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
Dude alisema kutokana na sheria za dini ya Kiislamu kwamba hairuhusiwi mwanaume kupikiwa futari na mwanamke anayeishi naye tu bila kufunga ndoa, amekuwa akiteseka kwenye suala la futari kwani mara nyingi anakula kwa mama lishe.
“Najuta kutofunga ndoa na mke wangu maana kila siku huwa nasema nitafunga leo mara kesho lakini miaka imekuwa ikikatika tu sijui kwa nini, kama mwezi huu mtukufu nakula futari kwa mama lishe huku nikiwa nalala chumba cha wageni mpaka mwezi huu uishe,” alisema Dude.
Dude amekuwa akiahidi mara kwa mara kwamba watafunga ndoa na mama watoto wake, Eva ambaye wanaishi pamoja na wamejaliwa kupata watoto wawili kwamba watafunga ndoa lakini suala hilo limegeuka kuwa kitendawili kwao.
[1.6MB]VIDEO CHAFU YA WANACHUO WA UDSM YAVUJA IONE HAPO CHINI =>
UNGANA NASI FACEBOOK KWA KULIKE PAGE YETU
Chapisha Maoni