Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania, Beatrice Singano Mallya akizungumza na waandishi wa Habari (hawapo pichani) katika mkutano uliofanyika katika ofisi za makao makuu ya Airtel jijini Dar Es Salaam mwishoni mwa wiki hii akiongelea mafunzo mbalimali yanayotolewa na “VSOMO” yaani VETA SOMO kufuatia uzinduzi wa mpango wa Airtel wa kijamii ujulikano kama AIRTEL FURSA wakishirikiana na Mamlaka ya Eimu ya Ufundi Tanzania (VETA) wiki moja iliyopita , ili kuwawezesha vijana kupata kozi mbalimbali zinazotolewa katika vituo vya VETA nchini kupitia simu za mkononi.
AIRTEL NA VETA YAWALETEA WANANCHI MFUMO WA KWANZA WA MAFUNZO YA UFUNDI KWA NJIA YA MTANDAO
- Kozi mbalimbali zapatikana kupitia application ya simu VSOMO
Vijana wa kitanzania wana kila sababu ya kufurahi kufuatia uzinduzi wa mpango wa Airtel wa kijamii ujulikano kama AIRTEL FURSA ikishirikiana na Mamlaka ya Elimu ya Ufundi Tanzania (VETA) kwa kuanzisha application hiyo ya “VSOMO” yaani VETA SOMO ulioanzishwa wiki moja iliyopita, ili kuwawezesha watanzania hasa vijana kupata mafunzo mbalimbali yanayotolewa katika vituo vya VETA nchini kupitia simu za mkononi.
Lengo la VSOMO ni kuweza kusaidia kupanua wigo wa mpango wa Airtel FURSA na kuwafikia vijana wengi zaidi hapa nchini katika kutoa elimu kwa njia rahisi na nafuu kwa wote. Mpaka sasa kozi zinazotolewa kutumia VSOMO ni ufundi pikipiki, ufundi umeme wa majumbani, ufundi wa simu za mkononi , ufundi Alluminium, utaalamu wa masuala ya urembo na ufudi wa kuchomea vyuma. Mafunzo haya yanapatikana kwa njia ya mtandao kwa wateja wote wa Airtel wenye simu aina ya android
Akizungumza na waandishi wa Habari katika ofisi za makao makuu ya Airtel jiji Dar Es Salaam mwishoni mwa wiki hii, mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano Mallya, alisema “matumaini ya mpango huu unaolenga kutoa mafunzo kwa vijana ili waweze kujifunza kutumia simu zao za mkononi na kuhitimu mafunzo ili kukuza biashara zao na kupata taaluma zitakazowawezesha kujiajiri wao wenyewe na hata kutoa ajira kwa vijana wengine.
Alisema kuwa mpango huu ambao unalengo la kufaidisha mamilioni ya Watanzania hususan vijana na kuweza kujifunza masomo mbalimbali ili kuendelea kuboresha kiwango cha elimu hapa nchini na kurahisisha upatikanaji wa elimu sambamba na kuboresha utendaji wa kazi kwa vijana wetu,”
“Ninaomba watanzania kuitumia vyema nafasi hii ili kuboresha elimu zao. Ninaamini kwamba kuanzia sasa watakuwa na muda mwingi wa kujisomea yote hii ikiwa ni kutokana na kurahisishiwa kwa kuweza kujisomea kupitia VSOMO . Jinsi ya kujiunga ni rahisi sana, mteja atatakiwa kupakua VSOMO kwenye orodha ya menu yake ya simu sehemu ya google play store na kujiandikisha bure bila gharama zozote. Mara baada ya kumaliza masomo yake kwa 40% mwanafunzi atatakiwa kwenda kwenye kituo cha VETA kilichopo karibu nae na kujiandikisha kwaajili ya mafunzo kwa vitendo ambayo yatachukua muda wa wiki 2 kumaliza ikiwa ni sawa na masaa 60 na ndipo atakapokaa kwajili ya mtihani na kutakiwa kufaulu kwa 60% “alisisitiza Mallya
Mallya alisema” Mwanafunzi atatahiniwa na kisha kuandikishwa na kutakiwa kulipia kiasi cha ada yenye punguzo shilingi 120,000/= kwa kupitia Airtel Money kwa kupiga *150*60#. Tunatoa wito kwa vijana kutumia fursa hii ya kipekee ili kupata mafunzo ya ufundi kwa urahisi na gharama nafuu kwani gharama ya masomo iko chini zaidi.”
[1.6MB]VIDEO CHAFU YA WANACHUO WA UDSM YAVUJA IONE HAPO CHINI =>
UNGANA NASI FACEBOOK KWA KULIKE PAGE YETU
Chapisha Maoni