Featured
Loading...

Waziri Mwigulu Atumbua Majipu Jimboni Kwake, Avunja Bodi ya Maji

MAAJABU YA MTANDAONI BOFYA HAPO CHINI HUTAAMINI MACHO YAKO =>
Waziri  wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Bw Mwigulu Nchemba akipokelewa na wananchi wa  Kata ya Tulia jimboni kwake Iramba jana.
Waziri Mwigulu akilakiwa na wapiga kura wake wakati wa mikutano yake ya kuwashukuru.
Waziri Nchemba akiwapungia mikono wananchi wake.
Waziri Nchemba akiteta jambo na mmoja kati ya walemavu katika Kata ya Tulia jimboni Iramba.
Waziri Mwigulu Nchemba akitangaza kuwasimamisha kazi viongozi wa bodi ya maji Mingela Iramba  kwa ufisadi wa mamilioni.
Waziri Nchemba akiwa na mmoja kati ya walemavu wa ngozi jimboni  kwake.

WAZIRI wa Kilimo Mifugo na  Uvuvi, Bw.  Mwigulu Nchemba amejitolea  kulipia kiasi  cha Tsh milioni 2 kwa kusaidia matengenezo ya mashine ya maji huku akitumbua majipu kwa kuwasimamisha kazi viongozi 15  wa  bodi ya maji ya kijiji  cha Mingela jimboni  kwake Iramba  wilaya ya  Iramba  mkoani Singida baada ya bodi hiyo  kufanya ufisadi wa milioni 9 za mradi wa maji wa  kijiji  hicho.
Viongozi hao ambao ni pamoja na Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Mingela, Mwenyekiti, Katibu, Mhasibu na wajumbe 12 ambao walikuwa  wakiunda bodi hiyo ya maji waliwasimamishwa baada ya kutafuna pesa hizo za mradi wa maji na kushindwa kulipia milioni 2 kwa ajili ya matengenezo ya mashine iliyoharibika .
Nchemba ambaye ni  Mbunge  wa Jimbo la Iramba alifikia uamuzi huo wa  kuivunja bodi hiyo ya maji kijijini hapo jana  baada ya  wananchi wa kijiji  hicho kulalamika katika  mkutano  wake  wa hadhara  kwa ajili ya  kuwashukuru kwa  kumchagua na kuanza kutimiza sehemu ya ahadi zake, kuwa hawana huduma  ya maji  safi baada kukosa Tsh milioni 2 za kutengeneza  mashine ya maji  iliyoharibika kwa  muda sasa.

Kutokana na kilio  hicho  cha  wananchi Nchemba  alilazimika  kumwita  jukwaani  Ofisa  Mtendaji wa  kijiji  hicho, Bw  Said Mussa na  bodi  yake  ili kueleza mapato na matumizi ya mradi  huo wa maji yapo kiasi gani na yapo  wapi, swali lililopelekea viongozi hao  kujichanganya kujibu kuwa ni kweli makusanyo ya mradi huo wa maji ni zaidi ya Tsh milioni 9.4 ila benki zipo  kiasi cha Tsh 400,000 na pesa  nyingine  zimetumika  kukarabati mashine hiyo iliyokuwa ikihitaji kutengenezwa kwa Tsh milioni 2 .
Mganganyiko  huu  ulimlazimu  waziri  huyo kuivunja bodi hiyo ya maji na  kumwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya  Wilaya ya Iramba,  Clement Berege kupeleka  wakaguzi  wa ndani mara  moja  katika  kijiji  hicho  ili  kukagua  mapato na matumizi  pamoja na  kuwachukulia hatua wahusika  wote  wa ufisadi   huo wa pesa za makusanyo ya maji.
Alisema  kuwa ni ufisadi mkubwa ambao umefanywa na viongozi hao wa bodi ya maji katika kijiji  hicho kwa  kutafuna  pesa  zote  pasipo matengenezo ya mashine ya maradi huo wa maji.
“Yaani  ni ufisadi  mtupu ambao  sikubaliani  nao hata kidogo mashine ya  kutengenezwa  milioni 2  imetengenezwa kwa  milioni 9 na bado haifanyi kazi …..naomba  wote  mliohusika na ufisadi  huu  kuanzia leo mkae pembeni na wakabidhiwe ofisi  watu wengine ……pia mkurugenzi kuanzia  sasa vitabu vyote vya makusanyo ya mapato vithibitiwe ili  kuepusha  kupoteza ushahidi ” 
Hata  hivyo  aliuagiza  uongozi wa Halmashauri  ya Wilaya  ya  Iramba  kutuma  wakaguzi wa ndani katika  vijiji vyote vya Halmashauri   hiyo  ili  kufanya  ukaguzi wa mapato na matumizi  kwenye vijiji  vyote.
Alisema  yawezekana  viongozi wa vijiji wamekuwa wakitumia vibaya makusanyo ya pesa za  wananchi bila  kufuata utaratibu wa kusoma mapato na matumizi kwa kila baada ya miezi  mitatu kwa  mujibu wa taratibu.
Katika  hatua  nyingine, Bw Nchemba aliutaka  uongozi wa  serikali za vijiji katika wilaya  hiyo ya Iramba kuacha  kuendelea  kuwatoza  wananchi  ushuru kandamizi wa biashara  ndogo  ndogo hasa  zile  zilizopigwa marufuku  wakati wa ugonjwa wa   kipindupindu  kwa kutoza ushuru  wa Tsh 10,000 kwa  biashara  ambayo mwananchi akiuza  yote faida  yake anaambulia Tsh 5000 hivyo  alishauri  uongozi wa Halmashauri kushusha  ushuru huo ambao ulikuwa maalum kwa mapambano ya ugonjwa wa  kipindupindu na kuwatoza ushuru wa Tsh 3500 kwa  wananchi  wanaojishughulisha kufanyabiashara ndogo ndogo ikiwemo ya upikaji pombe kwa ajili ya  kuendesha maisha  yao.
Pia  alitaka  wananchi  kuendelea  kudumisha usafi katika  biashara   zao  ili kuondokana na ugonjwa wa  kipindupindu, kwa  wananchi ambao walipatwa na maafa wakati wa mvua kubwa  zilizonyesha mwaka  huu, alisema  kuwa  wataalam  wa maafa  kutoka  ofisi ya  waziri mkuu watafika  kufanya tathimini ili  kuwasaidia  wananchi  hao.
Akijibu  tuhuma  hizo mbele ya  Waziri Nchemba, Ofisa Mtendaji wa Kijiji  cha Mingela, Bw  Said  Mussa alisema  kuwa ni kweli  walikusanya milioni 9.4  za mradi huo wa maji na fundi kutoka mjini Iramba anahitaji milioni 2 kwa ajili ya kutengeneza mashine hiyo ila kiasi  cha pesa kilichopo benki ni Tsh 400,000 pekee  hivyo hawana uwezo wa kulipia gharama  za fundi.
Alisema  kuwa kwa upande  wake hajui mhusika  halisi wa ufisadi  huo lakini kwa kuwa waziri amesimamishwa kazi  wote basi itasaidia  kumpata mhusika.
[1.6MB]VIDEO CHAFU YA WANACHUO WA UDSM YAVUJA IONE HAPO CHINI =>

UNGANA NASI FACEBOOK KWA KULIKE PAGE YETU

[1.6MB]HIZI NDIZO NJIA RAHISI ZA KUMRIDHISHA MSICHANA WAKO ZIONE HAPO CHINI =>

Chapisha Maoni

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright MFUKUNYUZI | Designed By Code Nirvana
Back To Top