Mkuu wa mkoa wa mara Magesa Mulongo amesema baada ya zoezi la wananchi kupewa muda wa kusalimisha silaha na kuhakiki kumalizika sasa msako wa nyumba hadi nyumba kuanza hivi karibuni.
Mulongo ameyasema hayo katika vijiji mbalimbali vya Mkoa wa Mara ambapo baada ya kuteuliwa na Rais Dkt. John Magufuli kuwa Mkuu wa Mkoa huo amekuwa akifanya ziara mbalimbali katika vijiji vya mkoa huo kwa lengo la kujitambulisha kwao na kuhimiza shughuli za maendeleo pamoja na kuelimisha wananchi juu ya utii wa sheria za nchi.
Mukongo ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa Mkoa wa Mara amewataka wananchi hao kusalimisha silaha kabla zoezi hilo la oparesheni halijaanza kwani halitaacha nyumba.
Aidha Mulongo amewatahadharisha viongozi wote wa vijiji ambao vijiji vyao matukio ya uhalifu wa mauaji na uvunjifu wa amani yanafanyika watambue watafikishwa kwenye vyombo vya dola kwa kushindwa kuwajibika katika kuwatumikia wananchi.
[1.6MB]VIDEO CHAFU YA WANACHUO WA UDSM YAVUJA IONE HAPO CHINI =>
UNGANA NASI FACEBOOK KWA KULIKE PAGE YETU
Chapisha Maoni