ABIRIA waliokuwa wakisubiri kusafiri kwa kutumia mabasi yaendayo kwa haraka eneo la Kamata-Kariakoo, Dar jana walijikuta wakilazimika kusubiri kwa zaidi ya saa 1 baada ya umeme kukatika kwenye eneo la kukata tiketi.
Tukio hilo lilizua sintofahamu kwa abiria hao ambao baadhi yao walitupa lawama kwa wasimamizi wa mradi wa mabasi yaendayo kwa haraka kwa kutoandaa mifumo yote inayohusika na usafiri huo kabla ya kuanza rasmi kutoa huduma.
“Muda wote tupo hapa tunasubiri umeme urudi ili tukate tiketi, sasa inakuwaje unaanza kutoa huduma wakati miundombinu yako haiko sawa?” Alisikika mmoja wa abiria aliyekuwa akisubiri eneo hilo.
Baada ya kusubiri kwa muda, baadaye umeme ulirejea na abiria wakaweza kukata tiketi na kuendelea na safari.
[1.6MB]VIDEO CHAFU YA WANACHUO WA UDSM YAVUJA IONE HAPO CHINI =>
UNGANA NASI FACEBOOK KWA KULIKE PAGE YETU
Chapisha Maoni