Featured
Loading...

Kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Mara yaagiza kukomeshwa kwa mauaji eneo la Nyamongo.

MAAJABU YA MTANDAONI BOFYA HAPO CHINI HUTAAMINI MACHO YAKO =>

Siku chache baada mwananchi mmoja kuuawa kwa kupigwa risasi katika eneo la Nyamongo wilayani Tarime, kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Mara imetembelea eneo hilo na kutoa maagizo mazito kwa vyombo vya ulinzi na usamlama wilayani humo kwa kutaka kukomeshwa mara moja mauaji hayo ya Mara kwa mara ikiwa ni pamoja na kudhibiti vitendo vya uvamizi wa mgodi huo wa North Mara unamilikiwa na kampuni ya Acacia Gold Mine.
Akizungumza baada ya kujionea uharibifu mkubwa ambao umefanywa na wananchi katika kituo cha afya cha Nyamongo wakati      wa vurugu kati ya polisi na wananchi muda mfupi baada mkazi mmoja wa kijiji cha Mrito kuuawa kwa kupigwa risasi, mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa mara Bw Magesa Mulongo, amesema haiwezekani wananchi kudai haki kwa kuvunjwa kwa sheria. 
Hata hivyo mwenyekiti huyo wa kamati ya ulinzi na usalama ambaye pia ni mkuu wa mkoa wa Mara, amemuagiza mkuu wa wilaya ya Tarime kuandaa mafunzo maalum kwa vikundi vya ulinzi wa jadi maarufu kama Seiga kwa kuzingatia sheria za nchi ili vitumike kwa shughuli za ulinzi katika eneo hilo. 
Awali viongozi na wananchi wa Nyamongo wamemuomba mkuu wa mkoa wa Mara kukubali sasa kurejesha kwa ulinzi wa kutumia vikundi vya jadi maarufu kama Seiga ambavyo wamesema vimekuwa na nafasi  kubwa ya kupambana na uhalifu katika eneo hilo.
[1.6MB]VIDEO CHAFU YA WANACHUO WA UDSM YAVUJA IONE HAPO CHINI =>

UNGANA NASI FACEBOOK KWA KULIKE PAGE YETU

[1.6MB]HIZI NDIZO NJIA RAHISI ZA KUMRIDHISHA MSICHANA WAKO ZIONE HAPO CHINI =>

Chapisha Maoni

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright MFUKUNYUZI | Designed By Code Nirvana
Back To Top